Al Iqlaab au Al Qalb [القَلب (الإِقلَاب)]

Maana ya Iqlab
Iqlaab katika luqha maana yake ni kubadilika. (Moyo katika lugha ya kiarabu ni Qalb kwa vile una kawaida ya kubadilika kutoka kwenye hali ya kuwa na imani na kwenda katika hali ya kutokuwa nayo). Maana ya ki-istilaah iqlab ni kubadilika kwa sauti ya nun kuwa meem na pia hutamkwa kwa ghunna.
Harufi ya Iqlaab
Iqlaab ina harufi moja tu, nayo ni baa (ب)
Iqlaab inavyotokea
Iqlaab hutokea iwapo nun sakina au herufi yenye tanwin itafuatiwa na harufi ya iqlaab yaani ب Iqlaab hutokea ama katika neno moja (لَيُنْبَذَنَّ) au baina ya maneno mawili (مِنْ بَعْدِ) yaani nun sakina au tanwin iko katika neno la moja na neno linalofuatiya linaanzia baa (ب). Vile vile katika baadhi ya misahafu huwekwa meem ndogo juu ya nun saakina kwenye iqlaab.
Iqlaab inavyotamkwa
Iqlaab hutamkwa kwa kubadilika kwa sauti ya nun na kuwa mim, hutamkwa kwa ghunna na hivyo kupelekea sauti ya meem kufichika. Ni lazima tuzingatie kwamba kinachobadilika ni sauti ya nun na sio katika kuandikwa, yaani kimaandishi nun saakina au tanwin hubakia kama ilivyo.

Rangi ya uanisho (Colour code)
Katika misahafu ya rangi (colour coded mus-haf) rangi ya bluu inayokooza, hata hivyo misahafu hutofautiana rangi.
Mifano ya Iqlaab


Suratil Layl, aya ya 8: Iqlaab ipo kwenye makutano ya nun saakina na baa baina ya maneno man na bakhila

  وَأَمَّا مَنْ بَخِلَ وَاسْتَغْنَى
  Suratil Humazah aya ya 4: Iqlaab ipo kwenye neno moja na lo ni layunbadhanna bina ya nun saakina na baa.
   كَلَّا ۖ لَيُنْبَذَنَّ فِي الْحُطَمَةِ

   Suratil Bayyinah, aya ya 4: Iqlaab ipo katika makutano ya maneno min na ba’di, ipo katika makutano ya nun saakina na baa

    وَمَا تَفَرَّقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَةُ

    Suratil ‘Alaq, aya ya 15: Iqlaab ipo baina ya ‘an fatha tain na baa, katika maneno lanasfa’an na binnaaswiyah.

     كَلَّا لَئِنْ لَمْ يَنْتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ

     Suratish Shams, aya ya 12: iqlaab inapatikana katika neno inba’atha, katika makutano ya nun saakina na baa.

      إِذِ انْبَعَثَ أَشْقَاهَا