Idghaam bila ya ghunna (إِدغَام بِغَيرِ غُنَّة)

Herufi za Idghaam bila ya ghunna
Idghaam hii ina herufi mbili kati ya sita za idghaam, nazo ni laam (لَام) na raa (رَاء)
Matokeo ya Idghaam bila ya ghunna
Iwapo Nun yenye saakina au herufi yenye tanwin itakuwa ni ya mwisho kwenye neno halafu neno linalofuatia likaanzia moja kati ya herufi hizi yaani laam (لَام) au raa (رَاء) basi itapatikana idghaam bila ya ghunna (إِدغَام بِغَيرِ غُنَّة)
Namna ya kutamka Idghaam bila ya ghunna
Sauti ya nun (ن) kutoka kwenye nun saakina au tanwin huunganishwa kwa ukamilifu kwenye laam (ل) au raa (ر) na hivyo sauti ya (ن) hupotea kabisa, vilevile hutamkwa bila ya ghunna.
Idghaam kamili (إِدْغَام قامِلَ) na Idghaam isiyokamilika (إِدْغَام نَاقِص)
Idghaam kamili (إِدْغَام قامِلَ) hupatikana kwenye makutano yafuatayo:-


1. Nun saakina au tanwin inapokutana na laam (ل) au raa (ر), sauti ya nun (ن) hupotea kabisa, juu ya hili wanazuoni wote wamekubaliana.

2. Nun saakina au tanwin inapokutana na nun (ن) au mim (م), ukamilifu wa muunganiko huanishwa kwa shadda (شَدَّة), au herufi inayounganishiwa (مُدْغَم فِيْه) (yaani kwenye laam (ل), mim (م) na nun (ن)). Kuhusu ukamilifu wa idghaam hizi, wanazuoni wengi wamekubaliana.


3. Idghaam isiyokamilika (إِدْغَام نَاقِص) hutokea iwapo nun saakina au tanwin inaunganika na herufi ya yaa (ي) au waw (و). Sababu ya idghaam hizi kutokamilika ni kwamba kwa asili herufi za yaa (ي) na waw (و) hazina ghunna na herufi ya nun ni yenye ghuna kiasili. Ndio maana mingi kati ya misahafu huwa shdda haiandikwi kwenye makutano haya kwenye herufi za yaa (ي) na waw (و)
Wanazuoni wamekubaliana kwamba nun saakina au tanwin inapokutana na baa (ب) au waw (و) hutokea Idghaam isiyokamilika yaani إِدْغَام نَاقِص kwa sababu muunganiko wa herufi hupungua au haukamiliki kwa sababu ya kuwepo kwa ghunna.
Mifano ya Idghaam bila ya ghunna (إِدغَام بِغَيرِ غُنَّة)
  1. Idghaam inapatika baina ya neno humazatin na lumazah
وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ
  1. Idghaam inapatikana baina ya maneno ‘iyshatin na raadhwiyah
فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ
Aya ya وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍ

Aya hii ambayo ni ya 27 ya suratil Qiyamah, haina idghaam isiyo na ghunna, yaani nun hutamkwa na hivyo hakuna idghaam kamili. Inaposomwa aya hii msomaji hana budi kusita baina ya neno man na raaq kusita huko ni kwa muda mfupi mno kiasi kwamba msomaji hatakiwi kupumua.