Maana ya Nun Saakina na Tanwin

Noon saakina (noon yenye saakin) ni noon isiyo mutaharrak (yaani haina fat-ha wala kisra wala dhumma), haibadiliki kwa namna inavyoandikwa wala kwa namna inavyosomwa ikiwa ni harufi ambayo utasimamia, yaani ikiwa ni herufi ya mwisho katika neno la mwisho kabla ya kusimama katika usomaji au hata ikiwa si herufi ya mwisho katika kusoma.Nun saakina inakuwepo kwenye nomino na vitenzi, pia inakuwepo katikati au mwisho wa neno. Nun sakina huandikwa na sukun mfano (مِنْهَا) au huandikwa bila ya alama ya sukun yoyote mfano (عَن)

Tanwin (fat-hatain, kisratain na dhwammatain) ni ainisho la nun ya ziada isiyotumika kwenye msisitizo. Tanwin hupatikana kwenye herufi ya mwisho ya nomino, nun hii katika nomino huwa haiandikwi lakini hutamkwa na huachwa kutamkwa iwapo msomaji anasimamia kwenye tanwin, yaani herufi yenye tanwin ni ya mwisho katika neno la mwisho kabla msomaji kusimama.


Noon saakina na (herufi yoyote yenye) tanwin kwa pamoja zina hukmu zenye kulingana, nazo ni hukmu nne:

الإِظهَار
الإِدغَام
القَلب
الإِخفَاء