Uandikaji wa Tanwin

Tanwin huandikwa kwa namna tofauti katika hukmu mbalimbali za nun saakina na tanwin.


1. Tanwin katika idh haar, fat-ha mbili, kisra mbili au dhwamma mbili hukaa sambamba na kulingana. Angalia fat-hatain kwenye waw ya kufuwan, kisratain kwenye shay-in na dhwammatain kwenye sawaaun.

  وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
  مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ
  سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَسْتَغْفَرْتَ لَهُمْ أَمْ لَمْ تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ لَنْ يَغْفِرَ اللَّهُ لَهُمْ


  2. Tanwin katika hukmu za Idghaam na Ikhfaa fat-ha mbili, kasra mbili au dhwamma mbili hupishana, yaani huwa hazikai sambamba.


   1. Tafadhali angalia kwenye msahafu katika Suratul Ibraahim (14) aya ya 31 fat-hatain kwenye Qaaf mwisho wa neno rizqan na kufuatiwa na neno lakum (Idghaam bila ya ghunna)
   2. Angalia kasratain ya mwisho wa neno raybin na kufuatiwa na neno mimma (Idghaam yenye ghunna)

   3. Tanwin katika hukmu ya Iqlaab fat-ha ya pili, kasra ya pili na dhwamma ya pili huandikwa kama meem (م) ndogo, kiasi cha ukubwa wa haraka. Angalia kwenye dhwammatain ya ‘ayn (ع) kwenye neno lanasfa’an (Iqlaab)

    لَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًۢا بِٱلنَّاصِيَةِ