Kuwafanyia Wema Wazazi

Allah sub-hanahu wa ta’ala amesema:
وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِنْدَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُلْ لَهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُلْ لَهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا [١٧:٢٣]
Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata  uff (yaani ah kwa wazungumzaji wa Kiswahili) Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. (17:23)
وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُلْ رَبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا [١٧:٢٤]
Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni. (17:24)
Maneno Muhimu
Rabb: Ni Mola aliyeumba na aliye mlezi wa vyote Ulimwenguni, Allah ‘azza wa jall.
Kuwafanyia wema wazazi wawili: kuwafanyia wema wazazi wawili ni amri ya Allah ambayo mara nyingi huja baada ya kuzungumzia kuabudiwa kwa Allah na kuepuka shirk.

أَبُو بَكْرَة رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : كُنَّا عِنْد رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ : أَلَا أُنَبِّئُكُمْ بِأَكْبَر الْكَبَائِر ثَلَاثًا الْإِشْرَاك بِاَللَّهِ وَعُقُوق الْوَالِدَيْنِ وَشَهَادَة الزُّور أَوْ قَوْل الزُّور ...
Amesema Abu Bakrah radhi Allahu ‘anh: Tulikuwa pamoja na Mtume salla Llahu ‘alayhi wa sallam akasema mara tatu: “Nikuambieni kuhusu madhambi makubwa; Kumshirikisha Allah, kutowafanyia wema wazazi wawili na kutoa ushahidi wa uongo au kusema uongo...”