Lengo La Kuumbwa

Tawhid imepewa kipaumbele cha hali ya juu katika Uislam kwa vile sababu ya msingi ya kuumbwa kwa binadamu ni kumuabudu Allah subhanahu wa ta’ala. Allah ta’ala  amesema katika surat Adh-dhaariyat:
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ [٥١:٥٦]
Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi (51:56)
Kutokana na aya hii hatuna budi kulielezea neno ibada. Ibada ni neno lenye maana pana, hujumuisha maneno pamoja na vitendo, vinafavyofanywa kwa uwazi au kwa siri ambavyo hulenga kumtukuza Allah ‘azza wa jall ili amridhie mja mwenye kufanya matendo (pamoja na maneno) hayo.

Mafunzo ya ya hii:-
  • Majini na binadamu huwajibika kufanya ibada zao zote kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah ta’ala tu.
  • Aya hii pia inaonesha lengo pekee la kuumbwa kwa binadamu na majini katika Ulimwengu.
  • Allah ta’ala pekee ambaye ana uwezo wa kuumba na hivyo yeye tu ndiye anayestahiki kuabudiwa bila ya mshirika wa aina yoyote.
  • Allah ‘aza wa jall ni mwenye kujitosheleza na hivyo si mwenye kuwahitaji viumbe wa aina yoyote katika lolote na viumbe wote ndio wenye kumuhitaji Allah ta'ala, hivyo majini na binadamu hunufaika wao katika kumuadu kwao Allah sub-hanahu wa ta’ala hapa Duniani na kesho akhera
  • Qur’an inashuhudia wazi juu ya uwezo mkubwa na busara za hali ya juu za Allah sub-hanahu wa ta’ala juu ya lengo zima la kuwaumba binadamu na majini.