Dua ya Sidja katika Sala

الَّهـُمَّ طَهِّرْ أَقْوَالَنَا مِنَ الَّغْوِ
Ewe Allah zitoharishe (zisafishe) kauli zetu kutokana na kauli za upuuzi.

وَأَعْمَالَنَا مِنَ العَبَثٍ
Na yasafishe matendo yetu kutakana na matendo yasiyo na maana

وَإِرَادَتَنَا مِنَ الوَهْنِ
Na nia zetu kutakana na udhaifu,

وَأَنْفُسَنَا مِنَ الشُّحٍّ
Na nafsi zetu kutokana na tamaa,

وَأَلْسِنَتَنَا مِنَ الكَذِبِ
Na ndimi zebu kutokana na uongo,

وَأَعْيُنِنَا مِنَ الخِيَانَةِ
Na macho yetu kutokana na khiyana,

وَقُلُوْبِنَا مِنَ النِّفَاقِ
Na nyoyo zetu kutokana na unafiki,

وَعِبَادَتَنَا مِنَ الرِّيَاءِ
Na Ibada zetu kutokana na riyaa (kujionesha),

وَحَيَاتَنَا مِنَ التَّنَاقُضِ
Na maisha yetu kutokana na utata.